1 day ago · MABAO matano yaliyofungwa na Shomari Kapombe, Jean Ahoua, Fabrice Ngoma na Steven Mukwala aliyepachika mawili, jana yaliirejesha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kupata ushindi wa 5-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo mkali wa aina yake uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.